1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Umma waomboleza kifo cha mwandishi

5 Juni 2005

Nchini Lebanon umati wa waombolezaji wakiwemo viongozi mashuhuri wa upinzani wamehudhuria mazishi ya mwandishi wa habari aliyekuwa akiushutumu vikali Syria.

Samir Kassir aliuwawa kutokana na mripuko wa bomu kwenye gari lake hapo Alhamisi.Kifo cha mwandishi makala huyo mwenye umri wa miaka 45 kimeifadhaisha Lebanon ambayo bado haikurudi katika hali ya kawaida kufuatia kuuwawa kwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Rafik Hariri hapo mwezi wa Februari.

Syria imekanusha kuhusika na mauaji hayo.

Wakati huo huo washirika wa Syria kundi la Hizbollah na Amal yanaonekana kujihakikishia ushindi leo hii wakati wakaazi wa Lebanon ya kusini wakijiandaa kupiga kura katika awamu ya pili ya uchaguzi wa bunge.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW