BEIRUT: Vikosi vya Lebanon vimepelekwa mpakani
23 Septemba 2006Matangazo
Wanajeshi wa kwanza wa Kilebanon wakisaidiwa na walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa,wameenezwa kwenye vituo vilivyo katika mpaka wa Lebanon na Israel.Kwa mujibu wa msemaji wa kijeshi,wanajeshi 400 wa Lebanon wakisaidiwa na vifaru,wamewekwa katika vituo vitano upande wa magharibi wa mpaka.Israel imechelewesha kuondosha vikosi vyake vyote mpaka kumalizika kwa mapumziko ya siku kuu ya mwaka mpya wa Kiyahudi,hapo Jumapili jioni.