1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Wanajeshi wa 800 wa jeshi la Italia wawasili Lebanon.

3 Septemba 2006

Kiasi cha wanajeshi 800 wa Italia wamewasili nchini Lebanon kushiriki katika jeshi lililoongezwa la umoja wa mataifa ambalo linakazi ya ulinzi wa amani kuyatenganisha majeshi ya Israel na yale ya Hizbollah.

Wanajeshi hao ni wa kwanza kuwasili katika jumla ya wanajeshi 3,000 ambao Itali imeahidi kutoa.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeidhinisha jeshi la wanajeshi 15,000. Ufaransa inatarajiwa kutuma wanajeshi 2,000 na Hispania itatuma wanajeshi 1,000.

Indonesia imesema kuwa itaanza kutuma wanajeshi wake 1,000 katika mwezi huu. Poland na Ubelgiji zimeahidi kutuma wanajeshi pia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW