1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Wanajeshi wa Lebanon wameanza kwenda kusini mwa nchi

17 Agosti 2006

Wanajeshi wa Lebanon wameanza kwenda katika eneo la kusini mwa nchi hiyo kuchukua nafasi zilizo kusini mwa mto Litani kama inavyotakiwa na azimio la Umoja wa Mataifa la kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la Hezbollah.

Wanajeshi elfu 15 watayakalia maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa na wanajeshi wa Israel.

Waziri wa fedha wa Lebanon, Jihad Azour, akizungumza juu ya kupelekwa kwa wanajeshi wa Lebanon katika eneo la kusini amesema, ´Tutahakikisha kwamba kupelekwa kwa jeshi la Lebanon katika eneo la kusini kutaongeza usalama wa raia wetu na kuidhibiti hali. Sio lengo letu kabisa kuutafsiri mzozo kati ya Israel na Lebanon kuwa mzozo wa ndani.´

Licha ya shinikizo la kimataifa, baraza la mawaziri la Lebanon limeliweka kando swala la kuwapokonya silaha wanamgambo wa Hezbollah, jambo mojawapo muhimu katika azimio la kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la Hezbollah.

Kufikia sasa Israel na Hezbollah zinaendelea kuliheshimu azimio la Umoja wa Mataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW