1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Wapalestina watakiwa kuweka silaha chini.

9 Oktoba 2005

Waziri mkuu wa Lebanon Fuad Siniora amekuwa na mikutano kadha ya mazungumzo na makundi ya wapiganaji wa Kipalestina katika juhudi za kumaliza kuwepo kwao na silaha katika makambi ya wakimbizi nchini humo.

Mikutano hiyo inakuja siku moja baada ya jeshi la Lebanon kuimarisha hatua za kiusalama kuzunguka vituo vinavyoendeshwa na wapiganaji wa Kipalestina wanaounga mkono Syria .

Wakimbizi 390,000 wa Kipalestina wanaishi katika makambi 12 nchini Lebanon , ambayo yanaendeshwa na wanaharakati wa Kipalestina , bila ya udhibiti wa aina yoyote wa viongozi wa Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW