Beirut. Watu maelfu kadha waondolewa Lebanon.
22 Julai 2006Matangazo
Zaidi ya watu 100,000 wanasemekana wameondolewa kutoka Lebanon katika muda wa siku chache zilizopita. Wengi wameondolewa kupitia katika bandari ya Beirut na kupelekwa nchini Cyprus na meli za kijeshi za Uingereza ama za Marekani, pamoja na meli za kawaida za Ugiriki, Italia na India.
Wizara ya mambo ya kigeni mjini Berlin imesema kuwa zaidi ya Wajerumani 4,200 wameondolewa hadi sasa.
Wengi wao waliondoka mjini Beirut na magari wakielekea Syria na Uturuki, ambako walipanda ndege na kurejeshwa Ujerumani na ndege za kivita pamoja na ndege za kukodi.
Lakini pia kuna taarifa kuwa baadhi ya Wajerumani ambao walikuwa likizo wamekwama katika maeneo ya vijijini.