1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut:Annan asisitiza kusimamishwa kwa mapigano Lebanon.

21 Julai 2006

Nchi kadhaa hivi sasa zinaendelea na zoezi lao la kutoa raia wao kutoka Lebanon.

Jeshi la majini la Marekani tayari limeshawahamisha kiasi ya raia wake 2,000 kupitia njia ya baharini, raia wengine zaidi wa Marekani wanachukuliwa hii leo.

Ujerumani tayari imeshahamisha raia wake kutoka Beirut kupitia Syria na Uturuki na hatimae kufika nchini Ujerumani.

Meli hiyo ya Marekani imechukua wafanyakazi 900 wa Umoja wa Mataifa na jamaa zao hadi Syprus ambako tayari kuna watu zaidi ya maelfu wakisubiri kupita njia ya kuelekea makwao.

Aidha Marekani imepinga kusikiliza makemeo kutoka mataifa ya nje ya kuunga mkono Umoja wa Mataifa wa kutoa wito wa kumalizwa vita ama kusimamishwa kwa mapigano huko Mashariki ya kati, kutuma misaada na kuruhusu mazungumzo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan jana alipeleka mapendekezo kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini Marekani ambayo ndio mkuu wa mpango wowote, imekataa kusimamishwa kwa mashambulizi.

Akizungumzia yale wanayoyahitaji kuhusu kusimamishwa kwa mapigano huko Mashariki ya kati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema

„ Jambo muhimu kabisa hivi sasa ni kumaliza uhasama kwa mambo matatu: Kwanza kusitisha mauaji ya watu wasio na hatia, mateso kwa raia. Pili, kuhakikisha misaada ya kiutu inawafikia inawafikia watu wote walio athirika, na tatu kutoa nafasi kwa mikakati ya kidiplomasia kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro unaoendelea“

Nae Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleeza Rice anategemewa kulizuru eneo la Mashariki ya Kati wiki ijayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW