BEIRUT.Israel yaondoa majeshi yake kutoka kusini mwa Lebanon
2 Oktoba 2006Matangazo
Lebanon imepandisha bendera yake katika mpaka wake na Israel baada ya vikosi vya kijeshi vya Israel kuondoka kutoka maeneo yaliyokaliwa na vikosi hivyo kwa mujibu wa makubaliano ya amani yaliyodhaminiwa na umoja wa mataifa.
Baadhi ya maeneo hayo yalikuwa chini ya ulinzi wa vikosi vya Lebanon miaka 30 iliyopita.
Vikosi vya kijeshi vya Israel vimeondoka kutoka kusini mwa Lebanon kufuatia kumalizika kwa vita baina yake na wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon.
Katika vita hivyo takriban Walebanon 1200 na Waisrael 157 waliuwawa.