Beirut:Israel yauwa 11 huko Lebanon.
28 Julai 2006Matangazo
Israel imeendeleza mashambulizi yake ya kijeshi huko Lebanon, na kuua kiasi ya watu 11, wakati ndege za kivita za Israel zilipoangusha mabomu katika kijiji kiliopo milimani nyuma kidogo ya kusini mwa bandari ya Tyre na mamia wakizunguuka kutaka kuvuka mpaka.
Vyanzo vya kiusalama vimesema, kiasi ya watu wanane, akiwemo raia mmoja wa Jordan wameuwawa , kutokana na mashambulizi ya anga 40 ya ndege za kivita za Israel.
Watu watatu nao wameuliwa kutokana na mashambulizi hayo hayo ya ndege mashariki mwa kilima cha Bekaa.