Beirut.Jeshi la Ujerumani liko tayari kuanza kazi ya doria.
15 Oktoba 2006Jeshi la majini la Ujerumani liko tayari kuanza kazi ya kulinda pwani ya Lebanon ikiwa ni jumla ya vikosi vya jeshi la kulinda amani la umoja wa mataifa UNIFIL.
Sherehe za uzinduzi wa kazi hiyo zinatarajiwa kufanyika leo katika meli ya kubebea ndege za kijeshi ya Italia , Garibaldi, ambayo kwa hivi sasa imetia nanga katika bandari ya Beirut nchini Lebanon.
Jeshi la majini la Ujerumani linachukua nafasi ya jeshi la Italia na Ufaransa ambayo yamekuwa yakilinda pwani ya nchi hiyo chini ya makubaliano ya azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa ambalo limemaliza vita vya siku 34 kati ya Israel na wapiganaji wa Hizboullah nchini Lebanon.
Ujerumani imetuma wanajeshi 2,400 nchini humo ikiwa ni ujumbe wake wa kwanza wa kijeshi katika mashariki ya kati tangu vita vikuu vya pili vya dunia.