BEIRUT:Jumuiya ya kimataifa yajitazizi kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa Lebanon
20 Oktoba 2007Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa,Italia na Uhispania wanakutana na viongozi wa Lebanon hii leo kujadili mzozo wa kisiasa unoendelea unaotishia kuzuia uchaguzi wa urais nchini humo.
Bernad Kouchner,Massimo D’alema na Miguel Angel Moratinos wanakutana na waziri mkuu Fuad Siniora spika wa bunge Nabih Berri na kadinali Nasralla Sfeir ambaye ni kiongozi mwenye usemi mkubwa katika jamii ya wakristo nchini Lebanon.
Hata hivyo vyombo vya habari vya Lebanon vimeripoti kwamba ziara hiyo ya siku moja ya viongozi hao wa nchi za magharibi haitafua dafu katika kurekebisha hali ya kisiasa nchini humo.Serikali ya waziri mkuu Siniora imelemazwa tangu upande wa upinzani ulipowandoa mawaziri wake sita katika serikali mwezi Novemba mwaka 2006 katika juhudi za kutaka kuwakilishwa zaidi serikalini.