1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Maelfu ya watu waendelea kuondoka Lebanon

22 Julai 2006

Wakati mapambano yanaendelea kati ya Hezbollah na wanajeshi wa Israel maelfu ya walebanon na wageni wanaendelea kuondoka nchini Lebanon na kukimbilia usalama katika nchi ya Uturuki na Cyprus.Wizara ya ulinzi ya Marekani imefahamisha kwamba raia wake 4,400 wameondolewa kutoka Lebanon.

Idara ya mambo ya nje mjini Berlin hapa Ujerumani imesema hadi sasa zaidi ya wajerumani 4200 wameondolewa kutoka eneo la mapigano,wengi wao wakipitia Syria na Uturuki na hatimaye kuletwa hapa nchini kwa ndege za kijeshi.

Lakini taarifa nyingine zinasema kwamba baadhi ya wajerumani waliokwenda kwa mapumziko kwenye eneo la vijijini nchini Lebanon hawajapata usaidizi wa kuondoka kutoka maeneo hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW