1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:majeshi ya Israel na ya Lebanon yapambana mpakani

8 Februari 2007

Majeshi ya Isreal na ya Lebanon yamepambana kwenye mpaka wa kimataifa wa nchi hizo, kwa mara ya kwanza tokea kumalizika vita vya siku 34 vya mwaka jana ambapo majeshi ya Israel yalipambana na wanamgambo wa Hezbollah.

Maafisa wa Isreal wamesema kuwa askari wao walishambuliwa wakati walipokuwa wanakagua mpaka kufuatia kugunduliwa mabomu manne kwenye mpaka huo .

Israel imedai kuwa mabomu hayo yaliyogunduliwa mapewa wiki hii, yalitegwa na wanamgambo wa Hezbollah.

Habari zinasema hapakuwa na madhara yoyote katika mapambano hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW