BEIRUT:Mapigano mapya Kaskazini mwa Lebanon
11 Juni 2007Matangazo
Mapigano makali yanaripotiwa kutokea tena katika kambi ya wakimbizi iliyo kaskazini mwa Lebanon.Jeshi la Lebanon linaendelea kushambulia maeneo yanayoshukiwa kuwa maficho ya wapiganaji wanaohusika na Al Qaeda.Mapigano hayo mapya yanatokea siku moja baada ya mapigano makali tangu Juni mosi wakati jeshi la Lebanon lilipoanzisha operesheni ya kuwafurusha wapiganaji wa Fatah al Islam.
Kulingana na afisa wa ngazi za juu wa kijeshi mpaka sasa wanajeshi 11 wamepoteza maisha yao.Serikali ya Lebanon inatia juhudi za kufanya majadiliano kuhusu suala hilo.