Beirut:Mapigano yaendelea katika kambi ya wapalestina Lebanon
16 Julai 2007Matangazo
Mapigano makali yameendelea kwa kwa wiki ya nane leo katika kambi ya wapalestina iliozingirwa kaskazini mwa Lebanon.Tangu Ijumaa iliopita majeshi ya Lebanon yamekua yakiwashambulia kwa mizinga na hujuma za vifaru wanaharakati wenye mafungamano na Al Qaida katika kambi ya Nahr el-Bared karibu na bandari ya kaskazini ya Tripoli. Serikali ya Lebanon ya Waziri mkuu fuad Siniora ameimarisha wanajeshi katika eneo hilo, kuwalazimisha wapiganaji hao wa msimamo mkali wajisalimishe. Kiasi ya watu 200 wakiwemo wanajeshi 100 wa Lebanon wanaripotiwa wameuwawa katika mapigano hayo ya miezi miwili sasa.