1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut:mashambulizi zaidi huko Lebanon.

17 Julai 2006

Israel imeendeleza mashambulizi yake ya anga huko Lebanon ikilenga bandari ya Beirut, uwanja wa ndege wa kimataifa na makaazi ya Hezbollah huko kusini mwa nchi, kama kampeni yake ya siku sita katika nchi hiyo.

Raia wanane wameuwawa wakiwemo watano wenye uraia wa Canada na Lebanon wakati Israel ilipovurumisha mizinga katika jengo huko kusini mwa Lebanon.

Waziri wa mambo ya nje wa Canada amesema kuwa jumla ya raia wa Canada saba wameuliwa.

Vyanzo vya habari vya Lebanon vimesema kuwa katika mashambulizi mapya yaliyofanywa na Israel yamepelekea kuuwawa kwa raia 60.

Wakati mashambulizi yakifanyika huko Lebanon, Israel pia imelishambulia kwa bomu jengo la Wizara ya mambo ya nje ya Palestina kwa mara ya pili katika kipindi cha wiki moja.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema, sehemu moja ya jengo hilo la ghorofa nane iliporomoka; na kujeruhi watu waliokuwa karibu na eneo hilo.

Israel imedai kuwa jengo hilo hutumiwa na wanamgambo wa Hamas kupanga mashambilio.

Kuhusu mapiganayo hayo baina ya Israel na Lebanon, Waziri mkuu Ehud Olmert wa Israel alisema

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW