1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut:Mashambulizi zaidi yafanywa na ndege za Israel.

4 Agosti 2006

Ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulizi ya nguvu huko kusini mwa Beirut kwa lengo la kutaka jeshi lake liweze kudhibiti sehemu zinazoshikiliwa na Hezbollah.

Shirika la msalaba mwekundu la Lebanon limesema, kiasi ya raia watano wameuwawa na wengine 15 wamejeruhuiwa, wakati ndege hizo zilipolipiga madaraja kaskazini mwa Beirut.

Mapema kiongozi wa Hezbollah Sheikh Hassan Nasrallah imeonya kuwa endapo Israel wataingia zaidi ndani ya Lebanon watarusha maroketi yao huko Tel Aviv kama kujibu mashambulizi ya Israel.

Kundi hilo limesema wapiganaji wake wamewauwa kiasi cha wanajeshi watatu wa Israel huko kusini mwa Lebanon.

Aidha majeshi ya Israel yameripotiwa kujitayarisha kusonga mbele kaskazini mwa Lebanon kuuelekea mto Litani kilomita 20 kutoka mpakani.

Hapo jana kiasi cha wanajeshi wanane wa Israel wameuwawa kutokana na maroketi ya Hezbollah, idadi inayotajwa kuwa ni kubwa tangu kuanza kwa mzozo huo miezi mitatu iliyopita.