1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Mauaji ya Hariri kuchunguzwa na Umoja wa Mataifa

27 Mei 2005

Kiongozi wa Ujerumani wa kundi la Umoja wa Mataifa litakalochunguza mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq Hariri amewasili mjini Berirut.

Detlev Mehlis atakiongoza kikundi hichocha wachunguzi wasiopungua 40 wa kimataifa.

Hariri aliuwawa katika shambulio la bomu mjini Beirut mapema mwezi Februari.

Syria imeshutumiwa kuwa nyuma ya mauaji hayo.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kufanywe uchunguzi baada ya kugundua kwamba uchunguzi uliofanywa na jopo la wachunguzi wa Lebanon una mushkil.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW