1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut:Serikali ya Lebanon yaahidi kujilinda na mashambulizi.

21 Julai 2006

Israel imetoa amri kwa vikosi vyake vya kijeshi vya hakiba kuwa tayari ikiwa kutakwa na idadi kubwa ya wanamgambo katika safari yao ya ardhini kuelekea Lebanon.

Ndege za kivita za Israel zimekuwa zikiangusha ujumbe wa tahadhari kwa raia yeyote aliepo sehemu za mpakani kuondoka kwa haraka katika mji huo.

Waziri wa ulinzi wa Lebanon Elias al-Murr amesema, jeshi la Lebanon watajilinda kutokana na mashambulizi hayo.

Wakati huo huo jeshi la Israel limesema, limeshambulia zaidi ya sehemu 40 walizozilenga usiku uliopita na kudhoofisha njia za Hezbollah wanazozitumia kupita kurusha roketi zao.

Madai ya Israel kuwa wameteketeza nusu ya nguvu za Hezbollah yamepingwa na kiongozi wa wanamgambo hao,Sheikh Hassan Nasrallah.

Sheikh Hassan ameongeza kuwa, Hezbollah watakubali kuwaachilia wanajeshi wawili wa Israel, kwa sharti la kubadilishana wafungwa.

Hata hivyo Israel imelitupilia mbali ombi la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan la kusimamisha mashambulizi yake dhidi ya Lebanon.

Kiasi ya walebanon 330 na wa Israel 33 wameshafariki tangu kuanza kwa mzozo huo wa Mashariki ya Kati.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW