BEIRUT:uchaguzi wa rais waahirishwa nchini Lebanon
25 Septemba 2007Matangazo
Bunge la Lebanon limeahirisha kikao muhimu cha kumchagua rais hadi hapo tarahe 23 ya mwezi ujao.
Spika wa bunge bwana Nabih Berri amesema sababu ya kuahirisha kikao hicho ni kutotimia theluthi mbili ya wabunge,idadi inayohitajika ili kuweza kumchagua rais. Upungufu huo umetokana na hatua ya wabunge wanaofungamana na Syria kutoshiriki kwenye kikao.
Vyama vya upinzani vinakusudia kuzuia kuchaguliwa rais mwenye msimamo wa kuipinga Syria.