1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Ushindi wa Hizbolla na Amal katika uchaguzi wa eneo la kusini Lebanon

6 Juni 2005

Matokeo rasmi ya uchaguzi wa hapo jana nchini Lebanon hayajatangazwa lakini ,Hata hivyo Makundi ya Hizbollah na Amal ambayo ni washirika wakubwa wa serikali ya Syria yamejitangaza washindi wa uchaguzi huo .

Inakisiwa makundi hayo yamejipatia asilimia 80 ya kura na hivyo kuweka wazi kwamba muungano huo huenda ukanyakua viti vyote 23 vinavyogombaniwa katika eneo la kusini.

Uchaguzi mkuu nchini humo ndio wa kwanza kuwahi kufanywa tangu kuondoka kwa wanajeshi wa Syria.Uchaguzi huo utaendelea hadi juni 19.

Hata hivyo Changamoto kubwa zinazolikabili bunge jipya ni pamoja na azimio la Umoja wa Mataifa linalotaka kundi hilo la Hizbollah kuweka chini silaha zao na wito wa Syria wa kumtaka rais Emile Lahoud ajiuzulu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW