1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut:wanajeshi 11 wa Lebanon wauliwa na mashambulizi ya Israel.

18 Julai 2006

Mashambulizi ya ndege za kijeshi za Israel nchini Lebanon yameingia katika siku yake ya saba.

Shambulio moja lililenga katika kambi ya kijeshi ya Lebanon huko mashariki mwa Beirut na kuuwa wanajshi wa Lebanon 11.

Israel imesema, ililenga wapiganaji wa Hezbollah ambao wamewakamata wanajeshi wao wawili.

Wakati huo huo wanamgambo wa Hezbollah wameendelea kurusha maroketi huko kaskazini mwaIsrael, mengi yao yameangukia katika mji wa Haifa.

Watu watano wamejeruhiwa na roketi hiyo iliyopiga mji wa Safed.

Zaidi ya raia wa Lebanon 200 wameuliwa tangu kuanza mashambulizi ya Israel huko Lebanon siku ya Jumatano, wakati ni raia 24 tu wa Israel ndio waliofariki hadi sasa kufuatia maroketi ya wanaharakati wa Hezbollah.

Wakati hayo yakitokea waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema nchi yake itaendelea na mashambulizi dhidi ya Lebanon hadi pale wanajeshi wake watakapoachiliwa huru na kusimamishwa kwa maroketi ya Hezbollah.

Olmert ametoa maelezo hayo mbele ya ujumbe wa umoja wa mataifa uliomtaka kusimamisha mashambulio wanayoyafanya dhidi ya Lebanon.

Asilimia 86 ya kura ya maoni ya hivi punde inaonyesha kuwa wananchi wa Israel wanaunga mkono hujuma zinazofanywa na jeshi la nchi hiyo dhidi ya Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW