BEIRUT:Waziri mkuu wa Lebanon azitaka pande zinazopigana kukoma
16 Julai 2006Matangazo
Waziri mkuu wa Lebanon Fuad Siniora amewatolea wito kupitia televisheni wapiganaji kukomesha mara moja vita.
Bwana Fuad amesema ni lazima waisrael wakomeshe kile alichokiita kuwa adhabu kwa watu wote wa Lebanon.
Waziri mkuu huyo ameutaka Umoja wa Mataifa kuingilia kati na kukomesha mapigano yanayoendelea huku akiiomba Marekani kuitolea wito Israel isimamishe mashambulio yake dhidi ya Lebanon.
Takriban watu 80 wameuwawa nchini Lebanon tangu Israel ianzishe opresheni yake ya kijeshi dhidi ya Lebanon siku nne zilizopita.
Wakati huo huo mataifa ya kigeni yameanza kuwaondoa raia wake kutoka nchini Lebanon.