BEIRUT.Waziri wa ulinzi wa Ujeumani akutana na waziri mkuu wa Lebanon
3 Novemba 2006Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz-Josef Jung amekutana na waziri mwenzi wa Lebanon Elias Murr akiwa katika ziara ya siku tatu mashariki ya kati.
Jukumu la jeshi la Ujerumani katika kulinda pwani za Lenabon ndio mada iliyo tawala mazungumzo ya viongozi hao.
Waziri Jung amekutana pia na waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora kabla ya kuelekea nchini Israel ambako pia atafanya mazungumzo na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Amir Peretz katika mji wa Tel Aviv.
Mazungumzo yake na mwenziwe wa Israel yatazingatia tukio la ndege za Israel la kufyatulia risasi manowari ya kijeshi ya Ujerumani wiki iliyopita katika bahari ya Mediterranean.