MigogoroUlaya
Belarus, Urusi zakagua silaha za kimkakati za nyuklia
7 Mei 2024Matangazo
Belarus imesema imeanza ukaguzi wa kutathmini utayari wa vikosi vyake kuweza kutumia silaha za kimkati za nyuklia, katika wakati ambapo nchi hiyo ikijiandaa pia na mazoezi ya matumizi yasilaha za nyuklia na mshirika wake Urusi.
Hayo yameelezwa na Shirika la habari la serikali Belta, likinukuu kauli ya Waziri wa Ulinzi wa Belarus Viktor Khrenin aliyesema kuwa Rais Alexander Lukashenko ameamuru ukaguzi wa kushtukiza wa vikosi vinavyosimamia silaha hizo.
Katika hatua ya kukabiliana na mataifa ya Magharibi, Rais Lukashenko alisema mwezi uliopita kuwa "dazeni kadhaa" za silaha za kimkakati za nyuklia kutoka Urusi zilitumwa huko Belarus kufuatia makubaliano yaliyotangazwa mwaka jana kati yake na Rais Vladimir Putin.