1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBelarus

Belarus yafungua mashtaka dhidi ya kiongozi wa upinzani

18 Januari 2023

Kulingana na mashirika ya habari yanayomilikiwa na serikali nchini humo, miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Tsikhanouskaya ni pamoja na uhaini na njama ya kunyakua madaraka.

ARCHIV | Schweden | Swjatlana Zichanouskaja
Picha: Sergei Gapon/AFP/Getty Images

Belarus imefungua mashtaka dhidi ya kiongozi wa upinzani Sviatlana Tsikhanouskaya lakini bila ya uwepo wake.

Kulingana na mashirika ya habari yanayomilikiwa na serikali nchini humo, miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Tsikhanouskaya ni pamoja na uhaini na njama ya kunyakua madaraka.

Tsikhanouskaya aliwania urais mwaka 2020 dhidi ya kiongozi wa kimabavu wa Belarus Alexander Lukashenko.

Lukashenko alipata ushindi mkubwa kwenye matokeo rasmi ya uchaguzi huo, lakini Tsikhanouskaya na washirika wake walidai kulikuwa na udanganyifu.

Baada ya matokeo, maandamano makubwa yasiyo ya kawaida yalishuhudiwa katika nchi hiyo ambayo zamani ilikuwa mwanachama wa iliyokuwa muungano wa Soviet.

Kufuatia uchaguzi huo, alikimbilia Lithuania na kuwa kiongozi wa upinzani aliyeko uhamishoni.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter, ameyataja mashtaka dhidi yake kuwa hatua za dikteta aliyepoteza madaraka kulipiza kisasi.