1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Belarus yamuhukumu Mjerumani adhabu ya kifo

20 Julai 2024

Mjerumani anayetuhumiwa na Belarus kufanya uhalifu ikiwa ni pamoja na "ugaidi" na "shughuli za mamluki" amehukumiwa adhabu ya kifo nchini humo.

Urusi St. Petersburg | Vladimir Putin na Alexander Lukashenko
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko (kushoto) akipeana mkono na mwenzake wa Urusi Vladimir PutinPicha: Alexander Demianchuk/TASS/dpa/picture alliance

Taasisi yenye kujihusisha na ulinzi wa haki, Viasna Human Rights Centre imesema Rico Krieger, mwenye umri wa miaka 30, alihukumiwa chini ya vifungu sita vya kanuni za jinai za Belarus katika kesi ya siri iliyofanyika mwishoni mwa Juni.

Sehemu ya mashauri hayo yalifanyika kwa siri, tuhuma kamili dhidiyake hazikufahamika mara moja na shirika rasmi la habari la Belarus halikuripoti chochote kuhusu kesi yake.

Belarus ni nchi pekee ya Ulaya inayotekeleza hukumu ya kifo, ikiitumika hasa kwa uhalifu mkubwa kama vile ugaidi na uhaini.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW