1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBelarus

Belarus yasema inaungana na Urusi kwenye luteka za kijeshi

10 Juni 2024

Belarus imesema inashiriki katika hatua ya pili ya luteka za kijeshi na Urusi iliyoagizwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin ili kujiandaa kwa mazoezi ya kupelekwa kwa silaha za nyuklia.

Belarus | Jeshi
Mwanajeshi wa Belarus akililinda helikopta kwenye uwanja wa mafunzo ya kijeshi wa Asipovichy wakati wa luteka za kijeshi za Zapad 2017.Picha: Brendan Hoffman/Getty Images

Waziri wa Ulinzi wa Belarus Luteni Jenerali Viktor Khrenin amesema mazoezi hayo ni hatua madhubuti ya kuongeza utayari wa kutumia kile kinachoitwa "silaha za kulipiza kisasi."

Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi ya wapi wala aina za silaha zinazutumika katika mazoezi hao.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi mwezi uliopita ilisema inatumai kwamba mazoezi hayo yangepoza kile ilichokitaja kama "vichwa vya moto vya Magharibi" baada ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kutaja uwezekano wa kutuma wanajeshi wa Ulaya kupigana na Moscow nchini Ukraine.

Hatua ya kwanza ya mazoezi hayo ilifanyika kusini mwa Urusi mwezi uliopita, katika kile wachambuzi wa masuala ya nyuklia walisema ni ishara ya onyo kutoka kwa Putin kuzuia nchi za Magharibi kujihusisha kwa undani zaidi katika vita vyake nchini Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW