1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Belgrade. Afisa wa jeshi ajisalimisha, ili kushitakiwa The Hague.

9 Aprili 2005

Afisa wa kijeshi wa Kiserbia ambaye anashitakiwa kwa mauaji yaliyofanyika katika mji wa Srebrenica mwaka 1995 amejisalimisha kwa maafisa mjini Belgrade.

Vujadin Popovic ni Mserbia wa 11 kujitoa kwa viongozi katika muda wa wiki 10 zilizopita. Msemaji wa serikali ya Serbia mjini Belgrade amewaambia waandishi wa habari kuwa Popovic atapelekwa katika mahakama ya umoja wa mataifa ya uhalifu wa kivita mjini The Hague. Serbia imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya watuhumiwa wa uhalifu wa vita ili kuwavutia kujitoa wenyewe kwenda kushitakiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW