1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bellingham ajiunga na Real Madrid kutoka Dortmund

14 Juni 2023

Mchezaji wa kiungo cha kati wa England Jude Bellingham amekamilisha uhamisho wake na kujiunga na miamba wa Uhispania Real Madrid kutoka klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga.

Jude Bellingham
Picha: Martin Meissner/AP/picture alliance

Bellingham ametia saini kandarasi itakayomuweka katika klabu hiyo hadi mwaka 2029. Taarifa kutoka klabu ya Real Madrid inasema mchezaji huyo nyota atazinduliwa kama mchezaji mpya wa klabu hiyo hapo kesho Alhamis.

Bellingham amejiunga na Madrid kwa bei ya zaidi ya yuro milioni100 na fedha hizo huenda zikaongezeka kutegemea na mafanikio atakayoyapata katika klabu hiyo ya Uhispania.

"Ilikuwa ni fahari kuivaa fulana ya Dortmund mara nyingi wakati wa mechi kubwa na hata ndogo. Ingawa nafurahia ninakokwenda, sitosahau safari niliyopitia kufika huko," alisema Bellingham.

Picha: Martin Meissner/AP/picture alliance

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 alijiunga na Borussia Dortmund kutoka Birmingham City ya Uingereza na akawa mchezaji muhimu wa BVB na msimu uliopita alipewa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga.

Chanzo: DPA

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW