1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bellingham hashikiki Uhispania

9 Oktoba 2023

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anasema hakuna aliyeterajia kwamba Jude Bellingham mwenye umri wa miaka 20 atacheza katika kiwango anachocheza sasa hivi.

Ligi ya Mabingwa Ulaya| Real Madrid - SSC Napoli
Mchezaji wa Real Madrid Jude BellinghamPicha: Francesco Pecoraro/Getty Images

Hii ni baada ya kung'ara kwa mara nyengine tena kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Uhispania Real Madrid walipopata ushindi 4-0 na Bellingham kufunga mabao mawili.

Bellingham amefunga mabao 10 katika mechi zake 10 za kwanza hapo Madrid na ameifikia rekodi iliyowekwa na Cristiano Ronaldo ingawa Bellingham amemshinda Ronaldo kwa kuwa amesaidia kuunda mabao mengine matatu, Ronaldo akiwa alisaidia kuunda bao moja tu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW