1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BENEFICA LISBON MABINGWA TENA NCHINI URENO-GAMBIA,GHANA NA I.COAST KUWAKILISHA AFRIKA KOMBE LA VIJANA LA DUNIA.

23 Mei 2005

BAYERN MUNICH NI MABINGWA DARAJA YA KWANZA NA

FC COLOGNE DARAJA YA PILI YA BUNDESLIGA

BENEFICA LISBON WATWAA TAJI LA URENO

GAMBIA NI MABINGWA WA KOMBE LA AFRIKA LA CHIPUKIZI.

NA GAMBIA,GHANA NA I.COAST KUWAKILISHA AFRIKA KATIKA KOMBE LA DUNIA LA VIJANA

Msimu wa mwaka 2004/2005 wa Bundesliga –Ligi ya Ujerumani ulimalizika rasmi jumamosi juku Bayern Munich ikivalishwa taji rasmi katika daraja ya kwanza na FC Cologne iklivaa taji katika daraja ya pili ya Bundesliga.Wakati taji la Munich lilikwisha julikana wiki 3 kabla kumalizika msimu, swali lilikuwa :ni timu gani zitaifuata Munich kunyakua tikiti za kucheza msimu ujao wa Champions League-Kombe la klabu bingwa barani Ulaya.Schalke ilimaliza nafasi ya pili na Bremen ikashika nafasi ya tatu ili kutwaa tiketi hizo.

Klabu tatu zinateremka daraja ya pili kutoka ya kwanza: nazo ni Freiburg,Hansa Rostock na Bochum.Klabu nyengine tatu zinapanda daraja ya kwanza :

FC Cologne ilioizaba jana Duisburg mabao 4:0 na kutawazwa mabingwa wa Bundesliga daraja ya pili.Duisburg na Cologne zilikwisha panda daraja ya kwanza kiasi cha wiki 2 nyuma. Swali likawa ni klabu gani ingechukua nafasi ya tatu:Kinyan’ganyiro kikawa kati ya Eintracht Frankfurt na Munich 1860.

Mwishoe, jana Frankfurt ilitamba na kuchukua nafasi hiyo ya tatu.Klabu 3 zilizopanda msimu uliopita kutoka daraja ya pili-Mainz,Armenia Bielefeld na Nuremberg zote zimeweza kubakia daraja ya kwanza.

Katika Ligi ya Ureno, Benefica Lisbon ilinguruma kama simba mwishoni mwa wiki ilipotwaa nayo taji lake la kwanza tangu kupita miaka 11.Benefica ilitoka sare jana bao 1:1 na Boavista na hii ilitosha kutoroka na ubingwa.

BARANI AFRIKA:

Timu 3 zitaiwakilisha Afrika katika kombe lijalo la dunia la vijana huko Peru hapo Septemba 15-nazo ni mabingwa wa Afrika Gambia,Ghana na Ivory Coast.Kufuatia finali ya Kombe la vijana la Afrika mwishoni mwa wiki, Gambia iliilaza Ghana bao 1:0.Katika kinyan’ganyiro cha kuania nafasi ya tatu Ivory Coast iliitimua Africa Kusini kwa bao 1:0.

Katika changamoto za Ligi mashuhuri za Africa, Enyimba ya Nigeria inaongoza baada ya kuitimua Lobi Stars mjini Aba jana kwa mabao 3-0.

Katika Ligi ya Ghana, Asante Kotoko imenyakua usukani wa Ligi kufuatia ushindi wa mabao 2:0 dhidi ya Hotspurs.

Katika Ligi ya Afrika Kusini,Kaiser Chiefs wamelinyakua tena taji la Africa Kusini jana kufuatia mabao 2 ya Collins Mbesuma katika lango la Bloemfontein Celtic.Kaizer Chief imeongoza Ligi kwa pointi 2 usoni mwa Orlando Pirates.

ASEC Abijan inaendelea kutamba bila kufungwa katika Ligi ya ivory Coast.ASEC imeilaza Satellite mabao 2-1 na inaongoza kwa pointi 12.

Nchini Zimbabwe, mabingwa CAPS UNITED wameilaza Dinamo 2-1 mjini Harare jana .Pigo hilo kwa Dinamo limeongoza kutimuliwa kwa kocha Sunday Marimo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW