1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki kuu ya dunia yazitaka nchi za Asia kupunguza mzigo wa ughali wa maisha kwa watu wake.

1 Aprili 2008

Washington.

Benki kuu ya dunia imezitaka nchi za kusini mwa Asia kuchukua juhudi za haraka kupunguza mzigo wa kupanda kwa bei za vyakula na mafuta kwa raia masikini wa eneo hilo. Ughali wa maisha unaleta changamoto kubwa kwa chumi za mataifa hayo kuliko hali ya mtafaruku wa masoko ya fedha , benki hiyo imesema katika ripoti yake ya nusu mwaka iliyotolewa leo.

Benki hiyo yenye makao yake makuu mjini Washington imesisitiza kuwa mataifa ya Asia yanahitaji kuendeleza hatua zake kuelekea kupatikana kwa viwango vya mabadilishano ya fedha vinavyokubaliana na mabadiliko, ili kuweza kupambana kwa hali bora zaidi na shinikizo la ughali wa maisha.

Tangu mwaka 2003, bei ya mafuta pamoja na bidhaa nyingi nyingine zimepanda kwa kiwango cha juu mno.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW