SiasaLibya
Benki Kuu ya Libya yasitisha shughuli, utekaji wa afisa wake
19 Agosti 2024Matangazo
Katika taarifa kwenye mtandao wa kijamii, benki hiyo imesema Musab Msallem ambaye ni mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari alitekwa nyara hapo jana na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.
Benki Kuu ya Libya imeongeza kuwa watendaji wengine wametishiwa kutekwa na kutoa wito wa kusitishwa kwa vitendo hivyo ambavyo imesema vinatishia usalama wa wafanyakazi wake na kukwamisha mwendelezo wa shughuli za sekta ya benki.
Libya yenye watu milioni 6.8, inatatizika kujikwamua kwenye mzozo wa miaka mingi baada ya vuguvugu la mapinduzi mnamo mwaka 2011 lililoungwa mkono na Jumuiya ya Kujihami NATO na kumpindua rais wa muda mrefu Moammar Gadhafi.