1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa waahidi ufadhili kukabiliana na saratani

6 Machi 2024

Wafadhili wa afya duniani wameahidi kutoa takriban dola milioni 600 kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

Mwanamke akipokea chanjo mjini Harare, Zimbabwe
Mwanamke akipokea chanjo mjini Harare, ZimbabwePicha: Jekesai Njikizana/AFP

Hayo yamesemwa katika kongamano la kwanza la kimataifa la kukabiliana na Saratani ya shingo ya kizazi, lililofanyika Cartagena, Colombia.

Katika taarifa ya pamoja, Benki ya Dunia, wakfu wa Bill na Melinda Gates na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, zimesema ufadhili huo utatumika kupanua upatikanaji wa chanjo, uchunguzi wa ugonjwa huo wa Saratani na matibabu duniani kote.

Soma pia: Mwamko wa wanawake kuhusu saratani ya kizazi ni mdogo

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema kwamba wana ujuzi na raslimali za kuangamiza ugonjwa wa Saratani lakini mipango iliyoko bado haijafikia viwango vinavyohitajika.

Ghebreyesus ameongeza kuwa kongamano hilo la kimataifa lilitoa fursa ya kubadilisha hali hiyo wakati serikali na washirika wa afya wa kimataifa wakijitolea kushirikiana kuangamiza ugonjwa wa Saratani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW