SiasaUkraine
Benki ya Dunia kuisaidia Ukraine kutathmini ya uharibifu
8 Juni 2023Matangazo
Mkurugenzi mkuu wa mipango katika ya Benki ya Dunia Anna Bjerde, amesema uharibifu wa bwawa la Novo Kakhovka umekuwa na matokeo mabaya kwa utoaji wa huduma muhimu pamoja na mazingira. Bjerde amesema tathmini hiyo mpya itajikita kwenye uharibifu wa miundombinu na majengo ya Ukraine, na kukadiria kuwa itagharimu dola bilioni 411 ili kufufua upya uchumi wa Ukraine baada ya uvamizi wa Urusi. Raia wa Ukraine wameendelea kuyahama makazi yao kutokana na mafuriko yanayoendelea kusini mwa nchi hiyo na yaliyosababishwa na uharibifu wa bwawa hilo huku Urusi na Ukraine wakiendelea kushtumiana kuhusika na tukio hilo.