Benki ya Dunia kuwalinda mashoga Uganda
16 Oktoba 2023Mkurugenzi wa Benki ya Dunia amesema wanakusudia kuhakikisha kuwa mashoga na wale waliobadili jinsia nchini Uganda hawatobaguliwa katika miradi ya taasisi hiyo, kabla ya kuanza upya ufadhili ambao ulisitishwa mwezi Agosti kutokana na sheria dhidi ya jamii ya wapenzi wa jinsia moja.
Soma zaidi: Umoja wa Mataifa wahofia uvunjwaji haki za binaadamu Uganda
Victoria Kwakwa, kiongozi wa Benki hiyo anayehusika na eneo la mashariki na kusini mwa Afrika, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa nyaraka za Benki ya Dunia "zinatowa msimamo wa wazi wa kutaka jamii ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda isibaguliwe na pia wafanyakazi watakaowajumuisha katika miradi hiyo wasikamatwe."
Kwakwa aliyasema hayo pembezoni mwa mkutano wa kila mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa ambao safari hii umefanyika katika mji wa Marrakesh nchini Moroko na kusisitiza kuwa serikali ya Uganda imeridhia matakwa hayo.
Mkopo wa Benki ya Dunia kwa Uganda mnamo mwaka 2022 ulifikia dola bilioni 5.2.