Benki ya Dunia yasitisha uhusiano na Tunisia
7 Machi 2023Katika tangazo lilochapishwa na Benki ya Dunia Jumapili jioni, rais wa benki hiyo David Malpass alisema kuwa matamshi ya Rais Saied yamechochea unyanyasaji wenye misingi katika ubaguzi wa rangi, na kwamba taasisi hiyo imeahirisha mkutano kati yake na Tunisia hadi itakapotangazwa vinginevyo.
Hata hivyo, kulingana na taarifa ambazo zimethibitishwa na shirika la habari la AFP, Benki ya Dunia itaendelea kuihudumia miradi iliyopo tayari nchini Tunisia.
Mwezi uliopita Rais Kais Saeid alidai bila kutoa ushahidi, kwamba ilikuwepo njama ya kubadisha utambulisho wa Kiarabu wa watu wa Tunisia kupitia uhamiaji wa watu kutoka Afrika ya kusini mwa jangwa la Sahara.
Baada ya matamshi hayo, wahamiaji kutoka nchi za kiafrika walirudishwa nyumbani kuepuka ghasia dhidi yao.