SiasaUkraine
Benki ya Dunia kufadhili miundombinu ya nishati Ukraine
13 Aprili 2023Matangazo
Ufadhili huo wa dola 200 zitatumika kufanya matengenezo ya dharura katika transfoma, mashine za kupasha joto za kuhamishika pamoja na vifaa vingine muhimu vya dharura.
Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji wa benk hiyo Anna Bjerde, amesema kiasi cha dola bilioni 23 zimekusanywa kama ufadhili kwa Ukraine na kutokana na miundombinu ya nishati nchini humo kukumbwa na uharibifu wa dola bilioni 11 hivyo kunahitajika msaada wa haraka.
Soma pia: Urusi yazidi kuharibu miundombinu ya Ukraine
Katika miezi ya nyuma Kyiv iliripoti namna ambavyo vikosi vya Urusi vililenga miundombinu ya nishati ya Ukraine na kusababisha kukatika kwa umeme nchini kote, na kwenye matokeo ya uhaba wa chakula, joto na maji safi.