1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki ya Kfw yamimina kwa shimoni bila ya kujua mamilioni ya Yuro

Hamidou, Oumilkher18 Septemba 2008

Kishindo cha benki zilizofilisika chaitikisa benki moja ya Ujerumani

Benki ya KfwPicha: picture-alliance/ dpa



Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi na mkasa unaozusha mabishano wa benki ya Ujerumani inayotoa mikopo kwaajili ya ujenzi mpya-Kfw,kutuma mamilioni ya fedha katika benki iliyofilisika ya Lehman Brothers.Mada nyengine ni kuhusu mjadala wa bunge la shirikisho Bundestag kuhusu bajeti na shambulio la kigaidi dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Sanaa nchini Yemen.


Tuanze na mkasa wa benki ya Kfw.Gazeti la HEILBRONNER STIMME linaandika:



"Lafontaine kaupata mkasa wa kuupigia domo;Benki ya serikali inayotoa mikopo kwaajili ya ujenzi mpya,imemimina "kwa makosa" yuro milioni 300 shimoni.Mtu atawaeleza vipi wakosa kazi wa muda mrefu -Herz nambari nne,au wanafunzi wanaolazimika kuketi katika darasa lililo chakaa?Kilichopotea sio tuu fedha,lakini imani ya watu kuelekea mfumo wa uchumi huru."



Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linajiuliza:



"Nani hasa wa kulaumiwa kama benki ya serikali inafanya makosa kama hayo?Kileleni mwa baraza la utawala la benki hiyo wanakutikana wanasiasa tangu wale wa mawaziri wa serikali kuu Steinbrück na Glos mpaka wale wa kiongozi wa chama cha mrengo wa shoto Die Linke-Oscar Lafontaine.Sawa kabisa kwamba walinzi wa shughuli za benki hawawezi kukagua kila shughuli za kibiashara za benki ya Bfw.Hata hivyo wanasiasa hao walikua wajue hali ikoje angalao tangu ilipotangazwa kwamba benki ya IKB imefilisika.Wangeweza kuzuwia pasitokee kosa lolote jengine.Badala yake Steinbruck ametumia kila fursa iliyojitokeza kudai kodi ya huduma za benki.Anaetaka kupigania kinga ya benki za kibinafsi anapaswa kwanza ahakikishe kwake mambo yanaendeshwa sawa sawa."



Gazeti la SCHWERINER VOLKSZEITUNG linahisi kiongozi mpya wa benki ndo wakulaumiwa.Gazeti linaendelea kuandika:



"Lawama za tangu awali kwamba benki ya mikopo ya ujenzi mpya imezibuaa lilipohusika suala la kuikoa benki ya IKB,kumbe hazikua za bure .Katika ya visa hivi viwili pamepita muda ulioshuhudia kuchaguliwa kiongozi mpya.Na ili Ulrich Schröder asije akapunjika baada ya kubadilisha kazi ,mshahara wake umeongezwa mara dufu kuliko ule wa mtangulizi wake.Kumlaumu yeye hivi sasa haitakua sawa kwasababu ndio kwamza wiki tatu zimepita tangu akabidhiwe hatamu za uongozi wa benki ya Kfw.Kwakua lakini anathamini fedha zake mwenyewe,analazimika kuwafichua nani wakosa na anabidi pia abadilishe mfumo mzimas ili kuepusha mikasa kama hiyo isije ikawaaibisha tena."



Na sasa tuigeukie mada ya pili magazetini:mashambulio ya kigaidi dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Sanaa nchini Yemen.Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linaandika:


"Hata kama rais Ali Abdallah Saleh wa Yemen si mwanademokrasia aliyekomaa,hata hivyo anajitahidi tangu miaka 30 ,kuimarisha umoja katika nchi hiyo inayozongwa na kuteketezwa kwa mivutano ya kikabila.Kazi yake imezidi kua ngumu tangu sehemu mbili za Yemen zilipoungana upya mnamo mwaka 1990.Wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam wanaitumia hali hiyo.Kwa kuendeleza mashambulio,wafuasi hao wa itikadi kali wanataka kuwatimua wamarekani toka Yemen.Wanaka pia kumdhuru rais Ali Abdallah Saleh wanaemuangalia kama kibaraka wa Marekani.Wafuasi wa itikadi kali wanajidai wanataka kuilinda Yemen, inayokutikana njia panda kati ya Afrika na Asia."


Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW