Bensouda aitaka Sudan kumkabidhi Haroun
3 Juni 2021Fatou Bensouda ataka mtuhumiwa huyo akabiliwe na mashitaka pamoja na afisa mwenzake wa zamani wa utawala.
Bensounda aliutoa wito huo jana Jumatano wakati wa mkutano na waandishi habari mjini Khartoum baada ya kufanya ziara ya kihistoria huko Darfur.
Ziara hiyo ni ya kwanza kuwahi kufanywa na mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya ICC tangu Umoja wa Mataifa ulipoipa jukumu mahakama hiyo kuchunguza mzozo wa Darfur miaka16 iliyopita.
Haroun ni miongoni mwa viongozi kadhaa wa utawala wa zamani waliokuwa na ushawishi mkubwa kushtakiwa na ICC kuhusiana na mzozi wa Darfur.
Wengine ni rais wa zamani wa Sudan Omar Hassan al Bashir, ambaye anakabiliwa na mshitaka ya uhalifu na mauaji ya halaiki, na Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman, kiongozi wa kundi la wanamgambo la Janjaweed.