BERLIN: Abiria kuathiriwa na mgomo leo
9 Agosti 2007Matangazo
Chama cha kutetea maslahi ya madereva wa treni hapa nchini Ujerumani kinapanga kutatiza usafiri wa treni katika miji ya Berlin na Hamburg katika mgomo utakaodumu kwa saa mbili wakati wa pilika pilika za kwenda katika shughuli za ujenzi wa taifa asubuhi leo.
Awali mahakama ya mji wa mashariki wa Chemnitz ilipiga marufuku migomo katika maeneo mengine nchini hapa.
Waziri wa biashara Michael Gloss amesema anaunga mkono uamuzi wa mahakama.
Chama kinachotetea maslahi ya madereva kinadai nyongeza ya asilimia 31 ya mishahara kwa wanachama wake.