1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Baraza la mawaziri wakuu wa majimbo laidhinisha katiba ya Umoja wa Ulaya.

27 Mei 2005

Ujerumani imekuwa nchi ya tisa katika muungano wa Umoja wa Ulya kuidhinisha katiba ya Umoja huo.

Wiki mbili baada ya bunge la shirikisho Bundestag, baraza la mawaziri wakuu wa majimbo ya Ujerumani Bundesrat limeidhinisha kwa wingi wa kura mkataba huo.

Jimbo pekee la Mecklenburgbh-Vorpommern linalo ongozwa na vyama vya SPD na PDS halikushiriki katika kura hiyo.

Chama kidogo cha PDS kinacho wakilishwa katika serikali ya muungano ya jimbo hilo la mashariki kinapinga katiba ya Umoja wa Ulaya.

Kura ya baraza la mawaziri wakuu wa majimbo ya Ujerumani Bundesrat imeswadifu siku mbili kabla ya wapiga kura wa Ufaransa kuamua kama wanaiunga mkono katiba ya umoja wa ulaya au la.

Utafiti wa maoni umeonyesha kuwa asilimia 55 ya wapiga kura nchini Ufaransa wanapanga kuipinga katiba ya umoja wa uklaya ambayo itafanya kazi tu ikiidhinishwa na nchi zote 25 wanachama.

Wakati huo huo kansela wa Ujerumani Gerhard Schröeder amesema nchi yake itatoa msaada kwa mataifa yanayoendelea ili yaweze kutumia rasilimali zake kwa njia bora na vile vile kuimarisha huduma za maji.

Amesema hayo katika siku ya pili ya mkutano wa kila mwaka wa wakirsto wa madhehebu ya kiprotestanti mjini Hanover.

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel bibi Wangari Maathai anatarajiwa kuhudhuria tamasha hiyo.

Zaidi ya watu laki moja walihudhuria siku ya kwanza ya tamasha hiyo huku askofu Wolfang Huber akisema kuwa vitabu na nyimbo za kumtukuza Mungu vinadhihirisha kuwa mwanadamu ameamua kurudi katika imani ya dini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW