1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Bunge lajadili bajeti

6 Septemba 2006

Baraza la chini la bunge la Ujerumani Bundestag liko tayari kuendelea na mjadala wake wa siku nne juu ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2007.

Kansela Angela Merkel anatazamiwa kufunguwa kikao hicho kwa hotuba juu ya bajeti.Hapo jana Waziri wa Fedha Peer Steinbrück amewaambia wabunge kwamba anategemea Ujerumani kutimiza masharti ya Mkataba wa Ukuaji na Uimarishaji wa Uchumi Barani Ulaya kwa mara ya kwanza tokea mwaka 2001.

Steinbrück amesema anataraji nakisi itakuwa kama asilimia 2.8 ya pato la jumla la ndani ya nchi ikiwa chini kidogo tu ya kiwango cha asilimia tatu kilichowekwa na mkataba huo wa Umoja wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW