BERLIN : Bunge lajadili ukosefu wa ajira
11 Machi 2005Matangazo
Baraza la chini la bunge la Ujerumani Bundestag limekuwa likijadili njia za kukabiliana na ukosefu mkubwa wa ajira nchini.
Hivi sasa watu milioni tano na laki mbili au asilimia 12.6 ya nguvu kazi nchini Ujerumani hawana ajira hiyo ikiwa ni rekodi ambayo haikuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha baada ya vita.Wapinzani wa kihafidhina wametowa wito wa kufanyika kwa mageuzi makubwa ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuregeza sheria za kazi.
Akizungumza katika baraza hilo la bunge kiongozi wa upinzani wa chama cha CDU Angela Merkel ameutangaza mpango wa vipengele kumi unaoitwa ‘Maafikiano ya Ujerumani’ ambao upinzani wanakusudia kuupendekeza kwa serikali wiki ijayo katika mazungumzo ya ngazi ya juu ya mgogoro huo wa ukosefu wa ajira.