1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN :CDU/CSU kuleta mabadiliko makubwa baada ya uchaguzi

12 Julai 2005

Vyama vya upinzani nchini Ujerumani vimesema , kwamba endapo vitashinda katika uchaguzi mkuu ujao ,vitaleta mabadiliko makubwa hasa katika sekta za kodi na ajira. Wenyeviti wa vyama hivyo bibi Angela Merkel wa chama cha CDU na bwana Edmund Stoiber wa chama cha CSU wameahidi hayo katika programu yao ya pamoja ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi wa septemba.

Vyama hivyo vinakusudia kuongeza kodi ya mauzo kwa asilimia mbili.

Mwenyekiti wa chama cha CDU bibi Merkel amesema kwamba lengo kuu litakuwa kutenga nafasi zaidi za ajira.

Hatahivyo chama kingine cha upinzani cha FDP kinapinga mpango huo wa kupandisha kodi kwa kuhoji kwamba ustawi wa uchumi utaathirika.

Wataalamu wa uchumi pamoja na jumuiya za wafanyakazi pia zinapinga mpango huo.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW