1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Chama cha SPD chakabiliwa na mzozo mwingine

28 Juni 2005

Chama kinachotawala nchini Ujerumani SDP kinakabiliwa na mzozo unaotokana na uamuzi uliopitishwa juu ya kuongeza kodi ya mapato ikiwa ni sehemu ya kampeni ya uchaguzi.

Mapato yatakayotokana na kodi hizo yataekezwa katika kuendeleza elimu na utafiti.

Kansela Schröder amesisitiza ulazima wa kodi hizo kwa kueleza kwamba, ikiwa mke na mume wana kipato cha Euro laki tano kwa mwaka basi watawajibika kutoa mchango wao katika kujenga mustakabali wa nchi yao.

Lakini waziri wake wa uchumi bwana Wolfgang Clement anapinga wazo hilo .

Bwana Clement ameeleza kwamba pendekezo lolote juu ya kuongeza kodi ni kosa.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW