1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Chama cha upinzani kinataka Uturuki kutoingizwa katika Umoja wa Ulaya.

27 Agosti 2005

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Ujerumani Angela Merkel amewataka viongozi wa vyama vya kihafidhina katika umoja wa Ulaya kujiunga nae katika kuipatia Uturuki, nafasi ya kuwa mshirika mpendelewa, badala ya kuipatia nchi hiyo uanachama kamili katika jumuiya ya Ulaya.

Katika barua aliyowapelea viongozi kumi wa Ulaya , Merkel amedai kuwa kuiingiza Uturuki katika jumuiya hiyo itakuwa mzigo mkubwa , kisiasa , kiuchumi , na kijamii.

Ameongeza kuwa uamuzi huo itahatarisha hatua ya muungano wa Ulaya. Merkel pia ameeleza juu ya upinzani wa Uturuki kuitambua jamhuri ya Cyprus kuwa ni kikwazo kwa Uturuki kuingia katika uanachama wa umoja wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW