BERLIN: Hakuna maafikiano kuhusu sera za serikali
5 Novemba 2007Matangazo
Serikali ya mseto nchini Ujerumani imeahirisha mkutano uliolenga kufumbua mizozo kadhaa ya sera, inayohatarisha umoja wa serikali hiyo.Makubaliano yanatazamiwa kupatikana katika kipindi cha juma moja lijalo.
Chama cha Kansela Angela Merkel cha CDU na chama ndugu CSU,vinaunga mkono sera zinazosaidia kukuza uchumi,wakati Kurt Beck anaekiongoza chama cha SPD anajaribu kuwazingatia wapiga kura wanaohisi kuwa wao,hawakunufaika kutokana na uchumi ulioimarika nchini Ujerumani.
Baadhi ya mada za mvutano ni kupunguzwa kwa malipo ya kodi,kurefushwa muda wa malipo ya ukosefu wa ajira kwa watu wazima,hadi ruzuku za ulezi wa watoto na kubinafsishwa shirika la reli la Ujerumani.