BERLIN: Hasara ya Euro milioni 50 kila siku moja
16 Novemba 2007Mgomo wa madereva wa treni unaoendelea siku ya tatu kwa mfululizo nchini Ujerumani,umewaathiri mamilioni ya wasafiri.Mashariki mwa nchi ni asilimia 20 ya treni tu zinazofanya kazi,wakati upande wa magharibi,takriban nusu ya treni zinaendelea kuwahudumia wasafiri.
Sekta iliyoathirika vibaya zaidi ni ya usafirishaji wa mizigo.Inatathiminiwa kuwa kila siku moja mgomo huo unasababisha hasara ya hadi Euro milioni 50.Waziri wa Usafiri wa Ujerumani, Wolfgang Tiefensee ametoa mwito kwa pande zote mbili kurejea kwenye meza ya majadiliano.Amesema:
O-TON TIEFENSEE:
„Misimamo ya vigeugeu ya kila upande kudai mapendekezo mapya,ikome.Badala yake,madai yaliyo mezani ndio yawe msingi wa majadiliano.“
Siku ya Jumatatu,chama cha wafanyakazi cha madereva wa treni-GDL kitaamua hatua ya kuchukuliwa kuhusu mgogoro huo wa madai ya nyongeza ya mshahara.Mgomo wa madereva hao, utamalizika Jumamosi asubuhi.